Pregnancy Aug 12, 2024

Kwa Nini Mama Mjamzito Hapaswi Kulala Chali?

Medikea Doctor

Medikea Doctor

Medical Expert

6960
Kwa Nini Mama Mjamzito Hapaswi Kulala Chali?

Mabadiliko mbalimbali wakati wa ujauzito hutokea katika afya ya mwanamke. Mabadiliko hayo husabishwa na uwepo wa mtoto kwenye mfuko wa uzazi pamoja na kuongeza kwa homoni

Mfuko wa uzazi huwa usawa wa kitovu ujauzito unapofikia wiki 20 na kuendelea. Uzito wa mtoto pamoja na ukubwa wa mfuko wa uzazi husababisha mgandamizo mkubwa kwenye mishipa mikubwa ya damu. Mishipa hii hutoa damu kwenye moyo na kusambaza sehemu za chini za mwili na mshipa mwingine hutoa damu sehemu za chini za mwili na kuirudisha kwenye moyo.

Mama mjamzito anapolala chali mfuko wa uzazi hukandamiza hiyo mishipa ya damu hivyo kupunguza uwezo wa kusafirisha damu. Kitendo ambacho husababisha shinikizo la damu (presha) kushuka. Hali hiyo husababisha mama kusikia kizunguzungu, kichefuchefu na hata kupoteza fahamu. Hali hiyo inaweza kuleta madhara makubwa kwa mama na mtoto aliyeko tumboni iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa .

Ili kuepuka madhara yatokanayo na hali hiyo mama yeyote mjamzito anashauriwa kulala upande wa kushoto ujauzito unapofika majuma 20. Kwa maswali zaidi kuhusu kizunguzungu and kichefuchefu cha mara kwa mara wakati wa ujauzito wasiliana na Daktari wa uzazi kupitia Medikea App.

Related Articles

Dalili za Mimba Wiki ya Kwanza
Pregnancy

Dalili za Mimba Wiki ya Kwanza

Ujauzito ni mchakato wa kibaiologia ambao unahusisha mabadiliko makubwa katika mwili wa mwanamke. Katika wiki ya kwanza, ...

31300
Feb 25, 2025
Read More
Jinsi ya Kupunguza Kichefuchefu na Kutapika wakati wa Ujauzito
Pregnancy

Jinsi ya Kupunguza Kichefuchefu na Kutapika wakati wa Ujauzito

Jifunze njia za kupunguza Kichefuchefu na Kutapika wakati wa Ujauzito⁣

12887
Aug 28, 2024
Read More
Je ni sawa kuendelea kunyonyesha mtoto wakati una mimba nyingine?
Pregnancy

Je ni sawa kuendelea kunyonyesha mtoto wakati una mimba nyingine?

Makala hii inaelezea kwa kina zaidi⁣

11187
Aug 28, 2024
Read More

More Health Insights

Saratani ya shingo ya kizazi
Women

Saratani ya shingo ya kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi inasababishwa na nini, dalili, na matibabu yake.

7998
Aug 29, 2023
Read More
Kupungua Kwa Kumbukumbu: Sababu Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo
Chronic diseases

Kupungua Kwa Kumbukumbu: Sababu Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo

Una wasiwasi kuhusu kupungua kwa kumbukumbu kwako au kwa mpendwa? Pata ushauri wa kitaalam kupitia application ya afya y ...

2254
Feb 25, 2025
Read More
Fahamu Sababu Za Kutokwa Na Damu Baada Ya Kufanya Mapenzi Au Kujamiiana
Women

Fahamu Sababu Za Kutokwa Na Damu Baada Ya Kufanya Mapenzi Au Kujamiiana

Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana yaweza kuleta wasiwasi ila pia ni kawaida. Zaidi ya asilimia 9% ya wanawake hupata ...

12006
May 4, 2024
Read More