Unapokwenda kumuona daktari huwa unajielezaje?
Medikea Doctor
Inawezekana umekwenda mara kadhaa kuonana na daktari kutokana na maradhi yanakusumbua. Lakini je umekuwa ukijieleza kwa sasa au umekuwa ukipata wakati mgumu kutoa maelezo yako kwa daktari.
Katika afya tunaamini kuwa hakuna kipimo chochote ambacho kimeweza kuchukua nafasi ya maelezo ya mgonjwa. Kwa maana nyingine ni kuwa maelezo yako kwa daktari ni muhimu sana katika kubaini ugonjwa wako.
Kwa kiasi kikubwa daktari anaweza kubaini ugonjwa wako kutokana na maelezo yako. Ni muhimu kutoa maelezo kwa ufasaha.
Ujieleze vipi?
Kumbuka unapokwenda kwa daktari una kuwa maradhi na sio ugonjwa. Ni wajibu wako kumueleza daktari maradhi yanakusumbua. Kutokana na maradhi yako ndipo daktari anaweza kujua unaumwa ugonjwa gani.
Maradhi ni tofauti na ugonjwa. Maumivu ya kichwa, homa, kichefuchefu, kutapika, kuharisha hayo ni maradhi. Wakati malaria, pneumonia, Kisukari hayo ni magonjwa.
Hivyo ukifika kwa daktari mweleze maradhi yako na sio ugonjwa.
Mfano mazungumzo ya mwazo baada ya salaam na utambulisho daktari anaweza kukuuliza
"Nini kimefanya uje hospitali leo au nini kimefanya uje kuniona"
Jibu lako linaweza kuwa: Ninasumbuliwa sana na maumivu ya kichwa leo siku ya tatu sasa. Unaweza kuongezea iwapo una dalili nyingine.
Epuka kutoa maelezo kama nimekuja kupima malaria au typhoid au presha. Maelezo kama hayo hayana msaada. Wasiliana na daktari kuirahisi kupitia App ya Medikea iliyopo Android na iOS.
Baada ya kuelezea maradhi yako makuu,maelezo mengine jibu kwa kadri daktari anavyokuuliza maswali.
Subscribe to Medikea newsletter
Sign up here to receive our wellness and health newsletters filled with actionable advice, from certified doctors, expert-vetted content, product recs, and more — delivered directly to your inbox.