Huu Ndio Utaratibu Wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji
Medikea Doctor
Kuwahi kutembea na kurudia shughuli za kawaida na za kabla ya ujauzito na kujifungua pamoja na mazoezi mara tu daktari anapoona ni salama inasaidia kuimarisha afya ya mama na kupunguza magonjwa yatokanayo na kukaa muda mrefu.
Hata hivyo wanawake wenye matatizo yafuatayo wanashauriwa kuchelewa kidogo kurudia mazoezi na shughuli za awali kabla ya ujauzito na wapate idhini ya daktari kabla ya kuanza kutembea au kufanya mazoezi
• Wenye magonjwa mengine (upungufu wa damu, magonjwa ya moyo na njia ya hewa, matatizo ya damu kuganda kwenye mishipa) • Wana maumivu na bado wanahitaji dawa za kutuliza maumivu • Madhara wakati wa na baada ya upasuaji (kichefuchefu na kutapika, kidonda kutopona vizuri, ganzi, mkojo kutoka wenyewe)
Sasa kwa wale ambao hawana matatizo na wale ambao wamepata idhini kutoka kwa daktari utaratibu wa kufanya mazoezi uko hivi :
▪️Wiki ya 1 hadi wiki ya 2 baada ya kuruhusiwa
Tembea angalau dakika 10 kwa siku mara nyingi kadri uwezavyo na unaweza kuongeza muda kadri unavyoweza
Panda ngazi nyumbani au hospital ukiwa na msaidizi
Usinyanyue kitu kingine chochote chenye uzito zaidi ya uzito wa mtoto
▪️Baada ya wiki 3 na kuendelea
Fanya mazoezi ya kuimarisha nyonga na tumbo
Angalia video za mazoezi yafuatayo YouTube (Pelvic tilting and abdominal curl,Lower back lift, Oblique curls, Lateral tilts, Kegel pelvic floor muscle). Fanya mazoezi katika kila kundi kuanzia mara 10 hadi 12 kwa kuanza taratibu na kuongeza kadri uwezavyo.
▪️Baada ya wiki 6 na kuendelea
-Wanawake ambao hapo awali walikuwa wanafanya mazoezi kwenye gym na vilabu vya mazoezi taratibu na kwa uangalifu wanaweza kurudia mazoezi yao kwa kuanza na settings za chini kwenye mashine za mazoezi
-Baada ya wiki sita wanawake wote wanaweza kufanya mazoezi ya kiwango cha kati (moderate intensity physical activity) kama inavyopendekezwa kwa watu wengine ambayo ni kufanya mazoezi hayo kwa muda wa dakika 150 hadi 300 kwa wiki)
Kwa msaada wa karibu wa mtaalamu wa mazoezi (Physiotherapist) pakua app ya Medikea ku chat au wasiliana na Medikea Clinic kupitia 0763100093 ili kupata mazoezi tiba clinic au nyumbani!
Subscribe to Medikea newsletter
Sign up here to receive our wellness and health newsletters filled with actionable advice, from certified doctors, expert-vetted content, product recs, and more — delivered directly to your inbox.