Je ni sawa kuendelea kunyonyesha mtoto wakati una mimba nyingine?

undefined

Medikea Doctor

Je ni sawa kuendelea kunyonyesha mtoto wakati una mimba nyingine?

Kuna wakati inatokea mama anakugundua kuwa ni mjamzito wakati bado ananyonyesha. Mtoto anayenyonyeshwa anaweza kuwa mdogo hajafikia umri wa kuachishwa au mama mwenyewe anakuwa bado anapenda kumnyonyesha mtoto wake. Ikiwa mimba ni ya kawaida na yenye afya, inachukuliwa kuwa ni salama kabisa kuendelea kunyonyesha katika kipindi chote cha mimba.

Katika kipindi hiki mama hana haja ya kuwa na wasiwasi kwamba maziwa yake yatakuwa hayana virutubisho vya kumtosha mtoto wake anayenyonya. Pia haitaji kuwa na wasiwasi kwamba unyonyeshaji unaweza kuathiri mimba yake.

Kuongezeka kwa uchovu na kichefuchefu wakati wa ujauzito inaweza kuwa changamoto kwa mama kijacho. Hata hivyo mama anashauriwa kupata muda wa kutosha wa kupumzika na kula mlo kamili. Ni muhimu kula mlo kamili ili kuhakikisha unapata virutubisho vya kutosha ili kukufanya uwe na afya njema.

Wakati wa ujauzito kiwango cha maziwa kinaweza kupungua pia radha ya maziwa huwa inabadalika. Mambo haya mawili yanaweza kusababisha mtoto mwenyewe kukataa kunyonya. Hata hivyo kama mtoto bado ni mchanga sana ni vizuri kuendelea kumnyonyesha ili asikose virutubisho muhimu kutoka kwenye maziwa ya mama.

Je wakati gani unashauriwa kumuachisha mtoto kama una mimba nyingine? Unaweza kushauriwa kuachishwa mtoto iwapo:

  • uko katika hatari ya kupata uchungu mapema,

  • mimba iko katika hatari ya kutoka au

  • daktari amekushauri USIFANYE tendo la ndoa wakati wa ujauzito.

  • Unapata maumivu ya tumbo yanayoambatana na kutoka damu

Zingatia:

  1. Ni muhimu kutumia njia za uzazi wa mpango ili kuepuka kupata ujauzito usiotarajiwa ili kuepuka madhara yatokanayo na ujauzito na uzazi. Na unaweza kuongea na daktari kujua njia bora ya uzazi wa mpango bora wakati unanyonyesha kupitia Medikea App.

  2. Ni muhimu kupata lishe Bora ili kuepuka kupata utapia mlo hivyo kujiweka katika hatari ya ujauzito wako kuharibika. Lishe ni MUHIMU, MUHIMU sana wakati huu.

Subscribe to Medikea newsletter

Sign up here to receive our wellness and health newsletters filled with actionable advice, from certified doctors, expert-vetted content, product recs, and more — delivered directly to your inbox.