Jinsi ya Kupunguza Kichefuchefu na Kutapika wakati wa Ujauzito
Medikea Doctor
Wanawake wengine hawapati matatizo yoyote wakati wa ujauzito, wakati wengine hukubaliwa na maradhi wakati wote wa ujauzito. Hata hivyo habari njema ni kwamba chochote kinachokusumbua, kuna njia za kukabiliana nayo.
Mojawapo ya maradhi yanayosumbua wajawazito wengi ni kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito. Bahati nzuri kuwa tatizo hili halisababishi madhara yoyote kwa mama wala kwa mtoto aliyeko tumboni.
Kichefuchefu hujitokeza kuanzia wiki nne hadi nane za mwanzo wa ujauzito. Kinaweza kuendelea hadi wiki 13 mpaka 14 za ujauzito. Wakati mwingine kichefuchefu kinaweza kuanza mapema zaidi na kuendelea kwa muda mrefu bila kukoma.
Nini husababisha kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito? Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kusababisha kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito. Hata hivyo ina hisiwa kuwa mabadiliko ya homoni yanatokea wakati wa ujauzito huenda yanasababisha hali hiyo.
Njia 7 za kupunguza kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito.
Kunywa maji mengi hasa baada ya milo. Usinywe maji mengi wakati wa kula.
Kula kidogo kidogo na mara kwa mara, epuka kula chakula kingi wakati mmoja.
Kula chakula kidogo wakati wa asubuhi kabla ya kuamka kitandani.
Epuka vyakula vyenye mafuta mafuta na vyakula vilivyokaangwa.
Tafuna au kunywa chai yenye tangawizi.
Lala na pata muda wa kutosha wa kupumzika
Kula vyakula vilivyokaushwa mfano cookies.
Iwapo hutopata nafuu baada ya kufanya hayo yote chati na daktari kupitia App ya Medikea na atakuandikia dawa ambayo inaweza kuzuia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito.
Subscribe to Medikea newsletter
Sign up here to receive our wellness and health newsletters filled with actionable advice, from certified doctors, expert-vetted content, product recs, and more — delivered directly to your inbox.