Women Sep 6, 2023

MIMBA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)

Dr Paul Masua

Dr Paul Masua

Medical Expert

7776
MIMBA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)

Hiyo ndio wataalam wanaita Ectopic Pregnancy.

MIMBA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)

Ni hali ambapo mimba inatunga nje ya uterasi au mfuko wa kizazi. Hali hii inasababishwa na ugonjwa wowote unaovuruga mirija ya mayai.

Mara nyingi mimba za nje ya kizazi huwa zinatungwa kwenye mirija ya mayai, hata hivyo mimba inaweza kutungwa sehemu yoyote katika tumbo ikiwemo utumbo au kwenye ini.

Hii ni hatari na inahitaji matibabu haraka.

SABABU ZA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI

  1. Magonjwa ya maambukizi: maambukizi ya mrija wa fallopian (pelvic inflammatory disease - PID), yanaweza kusababisha uharibifu wa mrija wa fallopian na hivyo kuongeza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi.

  2. Makovu au uvimbe kwenye Mirija: Inaweza kutokana na upasuaji wa awali kama vile upasuaji wa kutoa mimba ya nje ya kizazi au matibabu mengine kwenye kizazi.

  3. Endometriosis: Tishu zinazofunika kizazi (endometriamu) kukua nje ya kizazi

Sababu zinazoweza kuongeza uwezekano wa kupata Ectopic ni kama zifuatazo:

  • Historia ya awali ya kupata mimba nje ya kizazi
  • Kuvuta sigara au utumiaji Mkubwa wa pombe

Ni muhimu kuelewa kuwa sababu za mimba kutunga nje ya kizazi zinaweza kutofautiana kwa kila mtu na kwa hali ya kiafya. Ikiwa una wasiwasi au maswali kuhusu suala hili, ni vyema kuzungumza na daktari wako ili kupata ushauri wa kitaalamu.

DALILI ZAKE

  • Maumivu makali upande mmoja wa chini ya tumbo,
  • Kutokwa damu ya rangi ya nyekundu au nyeusi kwenye uke
  • Kizunguzungu
  • Uchovu
  • Mapigo ya moyo kwenda haraka

MATIBABU

Kwa sasa kuna matibabu ya aina mbili kulingana na hali ya mgonjwa kwa wakati huo ambayo ni dawa ama upasuaji, matibabu yote huwa yana matokeo sawa.

Iwapo mimba iliyotunga nje ya kizazi ikapasuka na mama akachelewa kupata matibabu kuna hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na damu kuvuja kwa wingi.

Kwahiyo kama wewe au rafiki ana dalili hizi, ni muhimu kuonana na daktari hata kwa njia ya simu kwanza, ili kufanya vipimo na kupata matibabu haraka iwezekanavyo.

Related Articles

Uti ni nini? Dalili zake na jinsi ya kujikinga
Women

Uti ni nini? Dalili zake na jinsi ya kujikinga

UTI inasababishwa na nini, dalili zake na jinsi ya kujinga

56439
Nov 6, 2024
Read More
Ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha
Women

Ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha

Soma kujua jinsi ya kuzalisha maziwa ya kutosha kwa mama anaenyonyesha!

3078
Aug 28, 2024
Read More
Huu Ndio Utaratibu wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji
Women

Huu Ndio Utaratibu wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

Huu Ndio Utaratibu Wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

5825
Aug 12, 2024
Read More

More Health Insights

MIMBA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)
Women

MIMBA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)

Umewahi kusikia mtu mimba imetunga nje ya mfuko wa kizazi?

7776
Sep 6, 2023
Read More
Saratani ya shingo ya kizazi
Women

Saratani ya shingo ya kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi inasababishwa na nini, dalili, na matibabu yake.

7827
Aug 29, 2023
Read More
Vyakula vitano vinavyosaidia kupunguza kiungulia
Nutrition

Vyakula vitano vinavyosaidia kupunguza kiungulia

Kiungulia ni hali inayotokea kwa watu wengi. Soma makala hii kujifunza zaidi.

16842
Aug 2, 2024
Read More