UTI NI NINI? DALILI ZAKE NA JINSI YA KUJIKINGA

Dr Saida Ally

Dr Saida Ally

UTI NI NINI? DALILI ZAKE NA JINSI YA KUJIKINGA

UTIs inaweza athiri mrija wa mkojo (urethra), kibofu cha mkojo na figo

MFUMO WA MKOJO

Mfumo wa mkojo ni mfumo wa mwili unaotumika kuondoa uchafu na maJi ya ziada

Mfumo huu unaundwa na ureta,kibofu cha mokojo,figo na urethra

UTI INASABABISHWA NA NINI?

Mara nyingi UTI zinasababishwa na bakteria aitwaye Escherichia coli (E. coli) na UTI nyingine zinaweza sababishwa na Chlamydia na Mycoplasma na UTI hizi zina athiri hadi mfumo wa uzazi na wanandoa au wenza wanapaswa kupata tiba pamoja.

Maambukizi ya UTI ni makubwa sana dunian Zaidi ya watu milioni 8.1 wanaathiriwa na ugonjwa huu.

DALILI ZA UTI

1.Kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa 2.Kuhisi kuunguzwa/kuwashwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo 3.Maumivu ya misuli na tumbo 4.Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia kubadilika rangi kuwa nyeusi au rangi ya mawingu nk 5.Kwa mtu aliyeathiriwa figo anaweza kuwa na maumivu mgongoni au kwenye mbavu pia kichefuchefu na kutapika 6.Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo.

NI WATU GANI WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UTI?

 • Watu wenye kutumia mpira wa mkojo kwa muda mrefu na pempas
 • Mtu yeyote mwenye tatizo katika mfumo wa mkojo kama vile kwenye figo,mirija inayosafirisha mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu , au kibofu
 • Baadhi ya njia za uzazi kama kutumia diaphragm,spermicides,kondomu nk
 • Tendo la ndoa linaweza likahamisha bakteria kutoka kwenye uke kwenda kwenye urethra
 • Wanawake ni wahanga wakubwa sana wa ugonjwa huu kulingana na maumbile yao ya nje

KWANINI WANAWAKE NDO WAHANGA WAKUBWA?

 1. Urethra(mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu) kwa wanawake ni mfupi sana hivyo kuruhusu bakteria kufika kwa haraka kwenye kibofu
 2. Pia mrija huo unafungukia sehemu ambazo zinaweza kuwa ni vyanzo bakteria ambayo ni sehemu ya uke na pili ni puru

Kwa wanaume ni vigumu sana ila wakipata tatizo linaweza kuwa zito kutibu tofauti na kwa wanawake

KWANINI UNAPATA UTI MARA KWA MARA (UTI SUGU)

 1. Mfumo wa kinga dhaifu: Mfumo wa kinga dhaifu unaweza kushindwa kupigana na bakteria wa kawaida wa UTI, kuruhusu maambukizi kurudiwa mara kwa mara.
 2. Kuwa mwanamke: Wanawake wana hatari kubwa zaidi ya kupata UTI kuliko wanaume kwa sababu urethra yao ni fupi, hivyo bakteria wanaweza kusafiri haraka hadi kwenye kibofu cha mkojo.
 3. Kukaa na mkojo kwa muda mrefu: Kukaa na mkojo kwa muda mrefu inaweza kusababisha bakteria kuwa na nafasi ya kutosha kujikusanya na kusababisha maambukizi.
 4. Ngono: Kujamiiana kunaweza kusababisha kuhamishwa kwa bakteria kutoka eneo la karibu hadi kwenye urethra.
 5. Kutokunywa maji ya kutosha: Kunywa maji ya kutosha husaidia kusafisha njia ya mkojo na kuondoa bakteria.
 6. Kutumia dawa za kuua bakteria mara kwa mara: Matumizi ya muda mrefu ya antibiotics au matumizi yasiyo sahihi ya dawa za kuua bakteria kunaweza kusababisha kuongezeka kwa bakteria wa kawaida wa UTI kuwa wa kawaida sugu.
 7. Mabadiliko ya homoni: Kwa wanawake, mabadiliko ya homoni katika kipindi kama vile ujauzito au baada ya menopausi yanaweza kuongeza hatari ya kupata UTI.
 8. Masuala ya kiafya: Hali kama vile kisukari, matatizo ya figo, au matatizo mengine ya kiafya yanaweza kuongeza hatari ya kupata UTI.

JINSI YA KUJIKINGA NA UTI

 1. Kunywa maji mengi kunasaidia kusafisha bakteria kwenye mfumo
 2. Mtu anatakiwa akojoe mara kwa mara kila anapojiskia kukojoa. Mkojo ukikaa sana kwenye kibofu unaweza zalisha bakteria
 3. Baada ya kukojoa wanawake wanatakiwa kujisafisha kuanzia mbele kurudi nyuma ili kulinda urethra
 4. Vaa nguo za ndani za pamba na ambazo hazibani sana kuruhusu hewa kupita vizuri ,epuka jinsi zinazobana sana ambazo zinaweza kukusanya na kuleta tatizo

ATHARI ZAKUTOKUTIBU UTI KIKAMILIFU

 • Uharibifu wa figo wa kudumu na kuhitaji huduma maalumu ya kutibu figo(dialysis)
 • Kutokea uwezekano wa kuzaa watoto wenye uzito mdogo au wanaozaliwa kabla ya wakati
 • Wanaume wanaougua UTI mara kwa mara wanakuwa kwenye hatari ya kupata madhara kwenye tezi dume (prostatitis)
 • Kusambaa kwa bakteria kutoka ndani ya figo na kuingia kwenye mfumo wa damu kusababisha sumu katika damu (sepsis)
 • Ikiwa unapata UTI mara kwa mara, ni muhimu kuongea na daktari wako ili kufanya uchunguzi wa kina na kupata ushauri wa matibabu sahihi. Daktari anaweza kutoa mwongozo kuhusu jinsi ya kuzuia UTI na matibabu yake.