ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha

undefined

Medikea Doctor

ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha

Uzalishaji wa maziwa unategemea kiwango cha homoni ya prolactin kinachopelekwa kwenye maziwa ya mama. Homoni ya prolactin inazalishwa kwa wingi kadri ziwa la mama linavyonyonywa mara nyingi au kukamuliwa mara nyingi. ⁣

⁣ Kwa hiyo siri kubwa kwa mama kupata maziwa ya kutosha ni kuhakikisha mtoto ana nyonya maziwa yake mara nyingi iwezekanavyo hasa siku za mwanzo baada ya mtoto kuzaliwa

Kama inawezekana hakikisha mtoto anaanza kunyonya ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa. Katika wiki tatu za mwanzo mtoto anapaswa kunyonya angalau mara 12 kwa siku. ⁣

Kuwahi kumuanzishia mtoto maziwa ya kopo kutaathiri uwezo wako wa kuzalisha maziwa, kwa sababu mtoto atashiba na hivyo kushindwa kunyonya. Kama mwanao anashindwa kunyonya kutokana na ugonjwa au sababu nyingine hakikisha mwenyewe unakamua maziwa yako.⁣

Endapo umemnyonyesha mwanao mara nyingi zaidi na unahisi hupati bado maziwa ya kutosha na mwanao hashibi unaweza kujaribu kutumia baadhi ya vyakula vinavyoongeza maziwa au ongea na daktari wako akuandikie dawa ya kuongeza maziwa. ⁣

Lakini zingatia: Jambo moja muhimu ni kuhakikisha mtoto ananyonya, mvutishe ziwa mara nyingi kadri uwezavyo, angalau mara 12 kwa siku katika kipindi cha wiki tatu za mwanzo. ⁣Kama utafanya hivi na bado unadhani maziwa hayatoshi, tafadhali wasiliana na mtaalamu wetu wa lishe kupitia Medikea App.

Subscribe to Medikea newsletter

Sign up here to receive our wellness and health newsletters filled with actionable advice, from certified doctors, expert-vetted content, product recs, and more — delivered directly to your inbox.