Watoto May 20, 2023

Manjano Kwa Watoto Wachanga: Sababu, Dalili za Hatari na Matibabu.

Medikea Clinic

Medikea Clinic

Medical Expert

4708
Manjano Kwa Watoto Wachanga: Sababu, Dalili za Hatari na Matibabu.

Manjano kwa watoto wachanga ni kubadilika rangi kwa ngozi na macho ya mtoto mchanga na kuwa ya njano. Hutokea kwa sababu ini la mtoto linakuwa halijakomaa vya kutosha ili kuondoa bilirubini kwenye mkondo wa damu.

Manjano ni hali ya kawaida hasa kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wao na baadhi ya watoto wanaonyonya katika wiki mbili za mwanzo wa maisha yao.

Sababu za manjano kwa mtoto mchanga:

  1. Kuzaliwa mapema: mtoto aliyezaliwa kabla ya wiki 38 huenda asiweze kuchakata bilirubin hivyo kusababisha ongezeko la bilirubin ambayo haijachakatwa (unconjugated/ indirect bilirubin). Hii hutokana na ini la mtoto mchanga kutokomaa hivyo kushindwa kuondoa bilirubin kwenye mkondo wa damu.

  2. Aina ya damu: ikiwa aina ya damu ya mama ni tofauti na mtoto , mtoto anaweza kuwa amepokea kingamwili kupitia kondo la nyuma ambalo husababisha chembe zake za damu kuvunjika haraka zaidi.

  3. Michubuko wakati wa kuzaliwa: mtoto anapopata michubuko wakati anazaliwa anweza kuwa na kiwango kikubwa cha bilirubin kutokana na kuharibika kwa seli nyekundu za damu.

  4. Ukosefu wa maziwa ya mama baada ya kichanga kuzaliwa au maziwa ya mama kutokuwa na lishe ya kutosha.

Dalili za manjano kwa mtoto mchanga:

Ngozi kuwa ya njano na weupe wa macho: unaweza kuangalia manjano kwa mtoto mchanga kwa kubonyeza kwa upole kwenye paji la uso au pua ya mtoto, na ikiwa ngozi inaonekana ya njano mahali ulipobonyeza basi kuna uwezekano kuwa mtoto wako ana homa ya manjano.

Wakati gani unapaswa kuwa na wasiwasi:

  • Ngozi ya mtoto inapokuwa ya manjano zaidi
  • Weupe kwenye macho ya mtoto unapoanza kubadilika na kuwa wa njano
  • Mtoto kuonekana mgonjwa na kuwa vigumu kuamka
  • Mtoto kutoongezeka uzito Mtoto kulia kwa sauti ya juu

Matibabu ya manjano kwa watoto wachanga:

Mara nyingi manjano ya kawaida kwa watoto wachanga hupotea yenyewe ndani ya wiki mbili au tatu. Ila kwa manjano ambayo ni kali,mtoto atahitaji kukaa kwa muda mrefu kwenye kitalu cha watoto wachanga au kurejeshwa hospitali.

Matibabu ya kupunguza kiwango cha bilirubini katika damu ya mtoto yanaweza kujumuisha:

  1. Lishe iliyoimarishwa na ya kutosha: hii husaidia kuzuia kupoteza uzito kwa mtoto.
  2. Tiba ya mwanga (phototherapy): ambapo mtoto huwekwa chini ya taa maalum ambayo hutoa mwanga katika wigo wa bluu-kijani. Mwanga huu hubadilisha sura na muundo wa molekuli za bilirubini kwa njia ambayo inaweza kutolewa kwa njia ya mkojo na kinyesi.
  3. Immunoglobulin ya mishipa (IVIg): kama sababu ya manjano ni tofauti za aina ya damu kati ya mama na mtoto. Kuingizwa kwa mishipa ya immunoglobulin (protini ya damu) ambayo inaweza kupunguza viwango vya kinga mwili, huweza kupunguza manjano na kupunguza hitaji la kubadilisha damu, ingawa matokeo si madhubuti.
  4. Kuongezewa damu: Mara chache, wakati manjano inapokuwa kali sana na matibabu mengine kushindwa kufanya kazi, mtoto anaweza kuhitaji kuongezewa damu, hivyo mtoto hutolewa kiasi cha damu mara kwa mara na kuibadilisha na damu ya wafadhili, kwa kufanya hivyo huweza kupunguza bilirubini na kinga mwili za mama.

MUHIMU:

Mtoto mwenye kiasi kikubwa cha manjano asipotibiwa anaweza akapata ulemavu wa kudumu katika ubongo wake kama vile mtindio wa ubongo, kupooza na ugumu wa kujifunza. Pia manjano iliyopita kiasi huweza kusababisha mtoto kupoteza maisha. Onana na daktari bingwa wa Watoto kupitia simu janja. Pakua app ya Medikea kwenye iOS au android.

Related Articles

Pumu Ya Ngozi Kwa Watoto: Visababishi, Dalili Na Matibabu
Watoto

Pumu Ya Ngozi Kwa Watoto: Visababishi, Dalili Na Matibabu

Pumu ya ngozi ni ugonjwa wa ngozi unaofanya ngozi kuwasha, kuvimba na kuweka viupele vidogovidogo vyenye rangi nyekundu ...

2980
May 15, 2024
Read More
Ugonjwa wa Pumu: Vihatarishi, Dalili na Matibabu
Watoto

Ugonjwa wa Pumu: Vihatarishi, Dalili na Matibabu

Je wajua? Katika Tanzania, pumu ni tatizo kubwa la afya ya umma. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 10% hadi 20% ya watoto ...

644
Feb 26, 2024
Read More
Tiba ya degedege kwa watoto
Watoto

Tiba ya degedege kwa watoto

Degedege, au kifafa, ni hali ya kiafya inayosababisha shambulio la ghafla na lisilo la kawaida la umeme katika ubongo.

2468
Jul 2, 2023
Read More

More Health Insights

Kupungua Kwa Kumbukumbu: Sababu Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo
Chronic diseases

Kupungua Kwa Kumbukumbu: Sababu Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo

Una wasiwasi kuhusu kupungua kwa kumbukumbu kwako au kwa mpendwa? Pata ushauri wa kitaalam kupitia application ya afya y ...

75
Feb 25, 2025
Read More
Tiba ya degedege kwa watoto
Watoto

Tiba ya degedege kwa watoto

Degedege, au kifafa, ni hali ya kiafya inayosababisha shambulio la ghafla na lisilo la kawaida la umeme katika ubongo.

2468
Jul 2, 2023
Read More
Kukatwa Mguu kwa Wagonjwa wa Kisukari Wenye Vidonda
Chronic diseases

Kukatwa Mguu kwa Wagonjwa wa Kisukari Wenye Vidonda

Zijue sababu za changamoto ya kukatwa miguu kwa wagonjwa wa Kisukari

310
May 20, 2024
Read More