Nutrition Aug 2, 2024

Vyakula vitano vinavyosaidia kupunguza kiungulia

Medikea Clinic

Medikea Clinic

Medical Expert

6561
Vyakula vitano vinavyosaidia kupunguza kiungulia

Kiungulia ni nini na kinasababishwa na nini? Kiungulia ni maumivu ya moto kwenye kifua, nyuma ya mfupa wa kifua. Maumivu haya hutokea baada ya kula, wakati wa kulala au wakati mtu ameinama.

Kiungulia hutokea wakati asidi ya tumbo inaporudi kwenye umio, mrija unaosafirisha chakula kutoka mdomoni hadi tumboni

KIUNGULIA KINAWEZA KUCHOCHEWA NA VITU KAMA VILE:

  • Vyakula vya mafuta au vya kukaanga.

  • Vinywaji vya kaboni, pombe, kahawa na vinywaji na vinywaji vya kafeini.

  • Bidhaa za machungwa.

  • Bidhaa za nyanya.

  • Chocolate

  • Milo mikubwa.

Ili kupunguza kiungulia inabidi kula vyakula vyenye asidi kidogo katika milo ya kila siku.

VYAKULA VITANO VINAVYOSAIDIA KUPUNGUZA KIUNGULIA

  • Vyakula vya alkali (Alkaline food): Vyakula hivi vina kiwango cha chini sana cha asidi hivyo husaidia kupunguza tatizo la kiungulia. Vyakula vya alkali huhusisha matunda kama vile ndizi na matikitiki, fenesi na karanga.

  • Tangawizi: Tangawizi ni mojawapo ya chakula cha asili kinachosaidia kupunguza tatizo la kiungulia. Tangawizi zina vitamin C na B, madini ya chuma, madini ya zink magnesium, calcium na phosphorus ambavyo pia hutumika kutibu tatizo la gesi tumboni na kiungulia.

  • Nyama zisizo na mafuta: Nyama kama vile kuku, bata mzinga na samaki hazina mafuta mengi hivyo zinaweza kutumika kupunguza hatari ya kiungulia kama zikichomwa au kuokwa. Hivyo ni vyema kuepuka kuzikaanga kwani vyakula vya kukaanga vina mafuta mengi na ni moja ya sababu kuu ya kiungulia.

  • Vyakula vya nafaka nzima: Vyakula vya nafaka nzima kama vile oatmeal, mkate na wali wa kahawia ni njia nzuri za kupambana na kiungulia kwani zinasaidia kunyonya asidi iliyojaa ndani ya tumbo, na nafaka hizi zimejaa vitamini na madini.

  • Maziwa mtindi: Maziwa ya mtindi ambayo hayana mafuta mengi husaidia kuzuia kiungulia na pia yana bakteria wazuri ambao huboresha usagaji wa chakula.

MUHIMU:

Ni vyema ukapata ushauri wa daktari kwanza kabla ya kuendelea na tiba yoyote ya mitishamba, kwa sababu vyakula vingine vinaweza kuwa na madhara kwako na mwingiliano wa madawa. Unaweza ku chat na daktari kupitia Medikea App.

Related Articles

No related articles found.

More Health Insights

Upungufu wa damu wakati wa ujauzito
Women

Upungufu wa damu wakati wa ujauzito

Zifahamu sababu za upungufu wa damu wakati wa ujauzito.

1780
Mar 12, 2024
Read More
Jinsi Ya Kuweka Malengo Halisi Ya Kupunguza Uzito
Afya na Siha

Jinsi Ya Kuweka Malengo Halisi Ya Kupunguza Uzito

This blog post in Swahili discusses how to set realistic weight loss goals using the SMART method and focusing on long-t ...

0
Mar 28, 2025
Read More
Je ni sawa kuendelea kunyonyesha mtoto wakati una mimba nyingine?
Pregnancy

Je ni sawa kuendelea kunyonyesha mtoto wakati una mimba nyingine?

Makala hii inaelezea kwa kina zaidi⁣

2980
Aug 28, 2024
Read More