SARATANI YA KIZAZI

Dr Living Kimario

Dr Living Kimario

SARATANI YA KIZAZI

NI NINI MAANA YA SARATANI YA KIZAZI?

Saratani ya kizazi ni aina ya saratani inayotokea kwenye utando wa ndani wa kizazi, uitwao endometriamu. Ni moja kati ya saratani zinazowakabili wanawake.

SABABU ZINAZOWEZA KUFANYA MWANAMKE KUWA KWENYE HATARI YA KUPATA SARATANI YA KIZAZI

 • Uzito kupita kiasi, 

 • Kukosa uwiano wa homoni (kama vile kuzidi kwa estrogeni), 

 • Wanawake ambao hawajawahi kuwa na ujauzito, 

 • Kuanza hedhi katika umri mdogo chini ya miaka 12, 

 • Kikomo cha hedhi (menopausi) kutokea katika umri mkubwa zaidi ya miaka 55

 • Historia ya saratani ya kizazi kwenye familia

DALILI ZA SARATANI HII

 1. Kutokwa na Damu baada ya kikomo cha hedhi 

 2. Maumivu Wakati wa Kujamiiana 

 3. Kupoteza uzito bila sababu inayojulikana 

 4. Kutokwa na Uchafu wa Muda Mrefu au Wa Kipekee: rangi ya kahawia au nyeusi, au uchafu wa kipekee ambao hauendani na mzunguko wa kawaida wa hedhi.

UCHUNGUZI WA SARATANI HII

 • Vipimo vya picha kama ultrasound, 

 • Vipimo vya tishu kama vile biopsy(kuchukua kinyama),

 • Kusafisha kizazi (D&C) ili kukusanya sampuli za tishu kwa ajili ya uchunguzi. 

MATIBABU 

Hutegemea hatua na aina ya saratani lakini zinaweza kujumuisha 

 • Upasuaji (kuondoa kizazi),

 • Tiba ya mionzi,

 • Chemotherapy, 

 • Tiba ya homoni, 

Ni muhimu kuonana na wataalamu wa afya kwaajili ya uchunguzi na miongozo binafsi ikiwa wewe au mtu unayemjua anaweza kuwa katika hatari au amegunduliwa na saratani ya utando wa kizazi.