Women Jan 27, 2024

Nini cha kufahamu kuhusu ugonjwa wa ukoma

Dr Kuduishe Kisowile

Dr Kuduishe Kisowile

Medical Expert

958
Nini cha kufahamu kuhusu ugonjwa wa ukoma

Tanzania ni kati ya nchi zinazopewa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu ambao historia yake inaturudisha karne nyingi zilizopita.

Mwaka 2020, jumla ya visa 1,208 vya ukoma viligundulika nchini, ambapo mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na kisiwa cha Unguja iliongoza kwa visa hivi.

Ukoma ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bakteria waitwao Mycobacterium leprae, wanaoshambulia mishipa ya fahamu. Maambukizi ya Ukoma ni kwa njia ya hewa pekee kupitia majimaji kutoka mfumo wa upumuaji wa mtu mwenye maambukizi ya Ukoma akipiga chafya au kukohoa. Tofauti na dhana potofu iliyosambaa kwa jamii nyingi, ugonjwa wa Ukoma hauambukizwi kwa kugusana au kushikana mikono.

Dalili za Ukoma:

  • Vijinundu kwenye ngozi
  • Baka au mabaka mwilini yenye rangi ya shaba yasiyo na hisia
  • Mishipa ya fahamu kuvimba
  • Ganzi kwenye mikono na miguu

Njia pekee ya kujikinga dhidi ya madhara ya Ukoma ni kwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na utambuzi wa mapema wa dalili zake ili kupata matibabu.

UKOMA UNATIBIKA! Iwapo mgonjwa wa ukoma atagundulika mapema, atapata matibabu ya dawa na kupona kabisa.

Tangu kuanzishwa kwa ugawaji wa dawa tiba za Ukoma kupitia Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma(NTLP) kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani(WHO), visa vya ukoma nchini vimepungua kutoka visa 35,000 mnamo mwaka 1983 hadi kufikia takribani visa 1,200 mwaka 2020.

Madhara ya Ukoma:

  • Misuli kukosa nguvu
  • Kupooza
  • Matatizo ya macho na kupelekea upofu
  • Ulemavu wa mikono na miguu

Kutokana na madhara ya Ukoma, waathirika wengi wa ugonjwa huu hunyanyapaliwa na kutengwa na jamii kwa hofu ya kuambukiza wengine. Tunapoadimisha Siku ya Ukoma Duniani, nitoe wito kwa jamii kuepuka kuwanyanyapaa waathirika wa ugonjwa huu na kuendelea kuchukua tahadhari. Iwapo utaona dalili mojawapo, wahi katika kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu nawe kwa matibabu zaidi.

Sources: NTLP, Wizara ya Afya, WHO Tanzania

Related Articles

Uti ni nini? Dalili zake na jinsi ya kujikinga
Women

Uti ni nini? Dalili zake na jinsi ya kujikinga

UTI inasababishwa na nini, dalili zake na jinsi ya kujinga

29693
Nov 6, 2024
Read More
Ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha
Women

Ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha

Soma kujua jinsi ya kuzalisha maziwa ya kutosha kwa mama anaenyonyesha!

467
Aug 28, 2024
Read More
Huu Ndio Utaratibu wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji
Women

Huu Ndio Utaratibu wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

Huu Ndio Utaratibu Wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

2266
Aug 12, 2024
Read More

More Health Insights

Probiotics: Je, Zinaweza Kuzuia au Kutibu U.T.I?
Chronic diseases

Probiotics: Je, Zinaweza Kuzuia au Kutibu U.T.I?

Probiotics na U.T.I.⁣

669
Oct 31, 2024
Read More
Je, ni sawa kufanya ngono wakati wa ujauzito?
Pregnancy

Je, ni sawa kufanya ngono wakati wa ujauzito?

Baada ya watu wengi kuuliza swali hili, ufafunuzi huu utasaidia watu wengi wawezi kufahamu.

1802
Aug 12, 2024
Read More
Dalili za awali za kisukari: Jinsi ya Kutambua na Kuchukua Hatua
Chronic diseases

Dalili za awali za kisukari: Jinsi ya Kutambua na Kuchukua Hatua

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa watu wengi hukosa fursa ya kugundua ugonjwa huu mapema kwa sababu ya kutojua da ...

100
Feb 25, 2025
Read More