Women May 4, 2024

Fahamu Sababu Za Kutokwa Na Damu Baada Ya Kufanya Mapenzi Au Kujamiiana

Medikea Clinic

Medikea Clinic

Medical Expert

3660
Fahamu Sababu Za Kutokwa Na Damu Baada Ya Kufanya Mapenzi Au Kujamiiana

Kwenye makala hii tutajibu maswali uliyonayo juu ya tatizo la kutokwa na damu baada ya kufanya mapenzi au kujamiiana na sababu mbalimbali na jinsi zinavyopelekea tatizo hili.

Je, ni kawaida kwa mwanamke kutokwa na damu baada ya kujamiiana?

Kutokwa na damu kwa kiasi kidogo mara baada ya kujamiiana huweza kuwa kawaida kama hutokea mara chache. Ila kama damu inatoka kwa wingi na ni mara kwa mara ni ishara ya tatizo la kiafya linalohitaji matibabu ya haraka, hivyo ni vyema kuwasiliana na mtoa huduma ya afya ili kufanyiwa vipimo na kapata matibabu stahiki.

Je, ni sababu zipi zinazopelekea kutokwa na damu baada ya kufanya mapenzi au kujamiiana?

Tatizo la kutokwa na damu baada ya kufanya mapenzi au kujamiiana huweza kusababishwa na mambo yafuatayo;

  • Ukavu wa uke; Tatizo la ukavu katika uke huweza kusababishwa na dawa za uzazi wa mpango zinazoathiri utengenezaji wa homoni ya estrojeni, kukoma kwa hedhi, msongo wa mawazo na mvurugiko wa homoni. Ukavu wa uke hupelekea michubuko wakati wa kujamiiana na kusababisha kutokwa na damu, pia huwa ni rahisi kuambukizwa magonjwa ya zinaa.
  • Maambukizi; Maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) kama vile klamidia na kisonono huweza kusababisha ugonjwa wa PID (Pelvic infalammatory) ambapo ugonjwa huu huathiri viungo vya uzazi na kushambulia sehemu za ndani za uke hivyo kupelekea tatizo la kutokwa na damu wakati au baada ya kujamiiana pamoja na maumivu ya nyonga, kutoka uchafu ukeni na harufu mbaya.
  • Udhibiti wa uzazi au uzazi wa mpango; wakati mwingine unapoanzisha njia mpya ya uzazi wa mpango huweza kupelekea kutokwa na damu wakati au baada ya kujamiiana. Hii husababishwa na kutumia vidonge vya udhibiti vya kiwango cha chini, kipandikizi au uke kuwa mkavu kutokana na udhibiti wa uzazi hivyo kusababisha kuchanika na kutokwa na damu wakati na baada ya kujamiiana. Baada ya miezi michache mwili huzoea na tatizo hili huisha.
  • Saratani ya shingo ya kizazi; Pia saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuwa sababu ya kutokwa na damu wakati au baada ya kujamiiana kwani uvimbe wa saratani huwa na mishipa mingi ya damu ambapo ukitokea msuguano na uume wakati wa kujamiiana huweza kupelekea kutoka kwa damu.

Nifanye nini tatizo la kutokwa na damu linapojirudia mara kwa mara?

Kama tatizo la kutokwa na damu wakati au baada ya kufanya mapenzi au kujamiiana limekuwa likijirudia mara kwa mara ni vyema kwenda kwenye kituo cha afya kwaajili ya vipimo na matibabu au unaweza kuchat na daktari moja kwa moja na kupata ushauri na matibabu stahiki kupitia Medikea App.

Related Articles

Uti ni nini? Dalili zake na jinsi ya kujikinga
Women

Uti ni nini? Dalili zake na jinsi ya kujikinga

UTI inasababishwa na nini, dalili zake na jinsi ya kujinga

25634
Nov 6, 2024
Read More
Ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha
Women

Ijue siri kubwa ya kuzalisha maziwa ya kutosha

Soma kujua jinsi ya kuzalisha maziwa ya kutosha kwa mama anaenyonyesha!

249
Aug 28, 2024
Read More
Huu Ndio Utaratibu wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji
Women

Huu Ndio Utaratibu wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

Huu Ndio Utaratibu Wa Kufanya Mazoezi Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

1865
Aug 12, 2024
Read More

More Health Insights

Nafasi Ya Usingizi Katika Kupunguza Uzito Na Namna Ya Kuiboresha
Afya na Usalama

Nafasi Ya Usingizi Katika Kupunguza Uzito Na Namna Ya Kuiboresha

Makala hii inaelezea umuhimu wa usingizi katika kupunguza uzito. Inafafanua jinsi usingizi unavyoathiri homoni za njaa, ...

0
Mar 28, 2025
Read More
Jinsi Ya Kuweka Malengo Halisi Ya Kupunguza Uzito
Afya na Siha

Jinsi Ya Kuweka Malengo Halisi Ya Kupunguza Uzito

This blog post in Swahili discusses how to set realistic weight loss goals using the SMART method and focusing on long-t ...

0
Mar 28, 2025
Read More
Vyakula 10 Vyenye Virutubisho Vingi Kwa Kupunguza Uzito (1)
Default